Home BIASHARAUWEKEZAJI Tanzania kuanzisha viwanda vya kutengeneza pikipiki

Tanzania kuanzisha viwanda vya kutengeneza pikipiki

0 comment 333 views

Serikali imesema inaendela kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha viwanda vingi vinaanzishwa nchini vikiwemo viwanda vya kutengeneza pikipiki.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji na kujenga miundombinu wezeshi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.

Kigahe ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda aliyeuliza mpango wa Serikali katika kuanzisha kiwanda cha kutengeneza pikipiki nchini.

Ng’enda amehoji “kutokana na matumizi makubwa ya pikipiki yanayofanyika nchini ni dhahiri upo umuhimu wa kuwa na kiwanda cha pikipiki, serikali haioni umuhimu wa kuvutia wawekezaji kwa kufanya juhudi maalumu ili mwekezaji aweke hapa ili kupunguza bei za pikipiki vijana waweze kumudu?.”

Katika swali la pili amehoji mkakati wa serikali wa kuwasaidia vijana kwa viwanda vinavyozalisha pikipiki ili zinapoingia nchni ziwe na bei ndogo.

Naibu Waziri Kigahe amesema kwa sasa kuna unafuu wa kodi kwa wafanyabiashara na baadhi ya watengenezaji ambao wanaleta pikipiki ambazo hazijaunganishwa na kuja kuunganisha hapa nchini tofauti na wanaoleta pikipiki kutoka nje.

“Hii inasaidia vijana wetu kupata ajira lakini pia kupata ujuzi ili hata baadae tukiwa na viwanda wawe wameshajua kuunganisha pikipiki,” ameeleza Kigahe.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter