Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Royal Tour yaongeza mapato kutoka Tsh 70bn hadi Tsh 84bn

Royal Tour yaongeza mapato kutoka Tsh 70bn hadi Tsh 84bn

0 comment 271 views

Ikiwa ni miaka miwili sasa ya filamu ya Royal Tour leo Mei 2, 2024 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi ameshiriki mahojiano maalum kupitia kipindi cha JANA na LEO kinachoruka kupitia Radio ya Wasafi Fm “live” kutoka katika Geti la Marangu, Mlima Kilimanjaro.

Dkt. Abbasi ameeleza mafanikio ya Filamu ya Royal Tour katika Mlima Kilimanjaro ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/24 Makadirio ya wageni ilikuwa ni 48,618 lakini hadi kufika Aprili 30, 2024 Hifadhi ya KINAPA imepokea wageni 53,739.

Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/24 makadirio ya mapato yalikuwa bilioni 78 hata hivyo hadi kufikia Aprili 30, 2024 mapato yameongezeka na kuwa zaidi ya bilioni 84.

Hivyo inaonesha kuwa filamu ya Royal Tour imelipa na inazidi kuinufaisha Tanzania.

Geti hilo ni mojawapo ya maeneo alikofika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifanya filamu ya “Tanzania: The Royal Tour.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter