Home WANAWAKE NA MAENDELEO Viongozi wanawake watakiwa kuweka mikakati kupunguza pengo la kijinsia umiliki akaunti za benki

Viongozi wanawake watakiwa kuweka mikakati kupunguza pengo la kijinsia umiliki akaunti za benki

0 comment 77 views

Viongozi wanawake wa mabenki wameaswa kuandaa na kutekeleza programu na mikakati itakayopunguza pengo la kijinsia kati ya wanaume na wanawake katika umiliki wa akaunti za Benki.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Sauda Msemo ameyasema hayo katika mkutano na viongozi Julai 18, 2024.

Mkutano huo ulilenga kujadili namna ya kuboresha huduma na bidhaa za kifedha zinazolenga wanawake nchini ili kuongeza ujumuishwaji wa wanawake katika sekta hiyo.

Aidha, ametaja uhaba wa elimu ya fedha, kukosekana kwa taarifa sahihi za wanaume na wanawake wanaotumia huduma za fedha (Gender Disaggregated Data) na sababu za kiutamaduni na hali duni ya kiuchumi kuwa miongoni mwa visababishi vya kuwepo kwa pengo hilo.

Pia, amewapongeza viongozi hao kwa kuendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanawake wanafikiwa na wanatumia huduma mbalimbali za kifedha.

Ripoti ya FinScope ya mwaka 2023 inaonesha asilimia 18 ya wanawake wana akaunti katika benki ukilinganisha na asilimia 27 ya wanaume.

Viongozi wanawake wa benki mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter