Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered nchini Sanjay Rughani amesema benki hiyo imejipanga kutumia kiasi cha Sh. 44.8 trilioni ili kuwezesha wafanyabiashara waendao nchini China ikiwa ni jitihada mojawapo ya kuimarisha biashara kati ya taifa hilo na Afrika.
Rughani amefafanua kuwa wafanyabiashara watakopeshwa fedha hizo kuanzia hivi sasa hadi mwaka 2020 kama mpango wa China kuimarisha ushirikiano na Tanzania ikiwa ni mbinu ya utekelezaji wa One Belt One Road Initiative.
Akizungumzia mpango huo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mkurugenzi wa maendeleo ya uwekezaji katika wizara hiyo Aristides Mbwasi amesema kuwa kuna kila sababu ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili wapate kufahamu fursa mbalimbali zilizopo na namna gani wanaweza kunufaika nazo.