Home BENKI Jinsi ya kufungua akaunti ya benki

Jinsi ya kufungua akaunti ya benki

0 comment 245 views

Katika ulimwengu wa hivi sasa, kuna umuhimu mkubwa wa kuweka akiba na kutunza fedha benki ndio njia salama zaidi ya kufanya hivyo. Watu wengi wamekuwa wakifungua akaunti kwenye benki mbalimbali lakini kuna wale ambao wamekuwa wakipata changamoto katika suala hili. Kama wewe ni mmoja wapo unaweza kufuata taratibu zifuatazo ili kufungua akaunti katika benki ya chaguo lako.

Fahamu ni benki gani unataka kufungua akaunti. Hii ni hatua muhimu sana kwani ukitambua benki gani inatoa huduma ambayo itasaidia kufikia dhamira uliyojiwekea, inakuwa rahisi zaidi kutunza fedha zako kwa malengo na kutimiza yale ambayo unatarajia kufanya hapo baadae.

Pili, ni muhimu kuwa na vielelezo ambavyo vitakutambulisha. Hakuna benki ambayo inatoa huduma hii bila kuwa na vitambulisho vya mteja. Vitambulisho hivi vinaweza kutofautiana kulingana na benki husika lakini mara nyingi utambulisho kutoka serikali za mitaa, kitambulisho cha kupiga kura, kile cha kusafiria (Passport) au cheti cha kuzaliwa hutumika. Ni vizuri kuwa navyo ukiwa unatarajia kufungua akaunti yako.

Tambua aina ya akaunti unayotaka kufungua. Kuna aina mbalimbali za akaunti, mara nyingi sio rahisi kufahamu ipi inayoendana na malengo yako bila usaidizi wa wataalamu wanaopatikana benki. Hivyo kama hauna uhakika,ni vizuri kuomba ushauri na kujifunza aina za akaunti zilzopo ili ufanye maamuzi sahihi.

Taratibu zote hizo zikikamilika, una nafasi nzuri ya kufungua akaunti yako pale utakapotembelea benki husika. Utajaza fomu maalum na kuweka vielelezo vyako, kuambatanisha picha na taratibu nyingine na baada ya kukamilisha yote hayo utafanikiwa kufungua akaunti yako kwa fedha kidogo tu ambazo mara nyingine hutofautiana kulingana na aina ya akaunti unayofungua pamoja na masharti yaliyopo katika benki ya chaguo lako.

Ni muhimu kwa jamii kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki pamoja na taasisi za kifedha kwani kama nchi ambayo inadhamiria kufikia uchumi wa kati, ni vizuri kwa wananchi wake kutumia njia za kisasa zaidi kutunza fedha zao hivyo hatua ya kufungua akaunti benki ni ya muhimu sana kwa watu wote.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter