Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Kuokota chupa kunawakalisha watu mjini

Kuokota chupa kunawakalisha watu mjini

0 comment 130 views

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao wamekuwa wakifanya biashara ya kuokota na kuuza chupa wanazookota mitaani. Wengi wanadai kuwa japokuwa kazi hiyo ni ngumu, inalipa na wanaweza kumudu maisha yao na yale ya familia zao kwa ujumla kupitia chupa hizi ambazo pengine wengine huona kama ni uchafu ambao hauna tena faida kwao.

Kawaida ya biashara hii ni kwamba waokotaji wa kawaida hukusanya chupa hizo na kuwauzia wanunuzi kwa kilo. Mara nyingi wanunuzi hawa hununua kwa jumla kwani wao wanauza viwandani ambapo chupa hizo hupokelewa kama malighafi na kuyeyushwa. Biashara hii hufaanyika sana katika miji kama Dar es salaam na baadhi ya nchi kama vile China na Kenya.

Wanaofanya biashara hii ya kuokota chupa mitaani wamesaidia kwa kiasi kikubwa katika suala la usafi kwani wapo makini kuhakikisha kuwa hakuna chupa inayozagaa ovyo mitaani. Licha ya hayo, ajira hii japokuwa sio rasmi imesaidia kupungua kwa vitendo vya uhalifu kwani vijana wamekuwa wakitumia muda wao kukusanya chupa baada ya kufanya vitendo hivyo.

Wengine wamekuwa wabunifu zaidi na kuunda vikundi vyao vya uajsiriamali ili kugawana majukumu pamoja na faida itakayopatikana. Wengine wamekuwa wakitafuta chupa kwenye madampo, wengine wamekuwa katika vituo vikubwa vya madaladala, wengine wanatembea mitaani ili mradi tu kuhakikisha wanatimiza wajibu walionao na katika kufanya hivyo wanaingiza kipato ambacho kinawawezesha kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.

Japokuwa watu wengi wameendelea kufanya kazi hii kama njia mojawapo ya kuwaingizia kipato, kuna athari ambazo hazipaswi kufumbiwa macho. Ajira hii ni hatari kwani inaweza kusababisha magonjwa mbalimbali. Watu wengi hawana vitendea kazi na hulazimika kutumia mikono yao bila kuwa na kinga ya aina yoyote. Hii ni hatari kwani wanaweza kupata maambukizi na wao pasipo kujua wakaambukiza watu wengine.

Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo wanapaswa kuwapa nguvu watu wanaofanya ajira hii ngumu kwa kuitambua kama kazi nyingine rasmi na kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya kufanya shughuli zao kwani wanabadili maisha yao na kujikwamua na hali ngumu ya maisha. Kupitia ajira hii wengine wameweza kusomesha watoto, kujenga na kujiendeleza hivyo wakiwekea mazingira bora zaidi ya kufanya kazi, mchango wao katika jamii utakuwa mkubwa zaidi ya ulivyo hivi sasa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter