Home FEDHA TRA kusamehe madeni kwa asilimia 100

TRA kusamehe madeni kwa asilimia 100

0 comment 100 views

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema mamlaka hiyo sasa ina uwezo wa kuwasamehe wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni kwa asilimia 100 tofauti na hapo awali ambapo Mamlaka hiyo ilikuwa na mamlaka ya kisheria ya kusamehe madeni kwa asilimia 50 pekee. Kichere amebainisha hayo wakati akitoa muongozo wa msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi wanayodaiwa wafanyabiashara mbalimbali.

 

Kamishna huyo ameeleza kuwa, lengo la msamaha huo ni kuwapa walipa kodi unafuu na fursa ya kulipa malimbikizo ya msingi ya kodi, pamoja na kuwapa hamasa ya kulipa kodi kwa hiari zao wenyewe na kwa muda unaotakiwa.

 

Bunge limepitia upya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 na sehemu ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015 na katika marekebisho, Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Mipango amepatiwa mamlaka ya kutoa utaratibu maalum wa kumwezesha Kamishna Mkuu kutoa msamaha wa riba na adhabu hadi asilimia 100, riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi tofauti na asilimia 50 ya hapo mwanzoni.

 

Kichere amefafanua kuwa msamaha huu utahusisha kodi zote zinazotozwa kwa mujibu wa Sheria chini ya TRA isipokuwa ushuru wa forodha uliopo chini ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter