Home BIASHARAUWEKEZAJI China kuwekeza trilioni 126/= Afrika

China kuwekeza trilioni 126/= Afrika

0 comment 118 views

Rais wa China Xi Jinping amesema nchi yake itatoa Dola bilioni 60 za Marekani (Sh.126 trilioni) kwenye mpango wake wa miaka mitatu ya ushirikiano na Afrika katika harakati za maendeleo. Rais huyo amesema hayo wakati akifungua mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) jijini Beijing. Jinping ameahidi kuwa China itaendelea kushirikiana na Afrika ili kudumisha amani ambayo amesisitiza ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.

Mbali na hayo, Rais huyo pia amesema China itaendelea kusaidia Afrika katika miradi kama vile ujenzi wa miundombinu, ushirikiano katika sekta ya biashara na pamoja na huduma za afya. Nchi ya China pia itatoa fursa za mafunzo ya kilimo na ufundi kwa wataalamu kutoka barani Afrika ili kuchochea maendeleo ya uchumi.

Katika maelezo yake, Rais Jinping amesema tofauti na miaka ya nyuma, anaamini kuwa ukaribu wa China na nchi za Afrika umeimarika na wamekuwa wakishirikiana kwa karibu zaidi katika shughuli za kimaendeleo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anamuwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo alipata fursa ya kusalimiana na kiongozi huo baada ya ufunguzi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter