Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji watakiwa kufuata sheria

Wawekezaji watakiwa kufuata sheria

0 comment 180 views

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani humo Jokate Mwegelo amewataka wawekezaji kufuata kanuni na sheria za uwekezaji zikiwemo ulipaji kodi bila shuruti kwa manufaa ya wawekezaji na taifa kwa ujumla.

Soma Pia Majaliwa akaribisha wawekezaji kutoka China

Mwegelo ameyasema hayo katika kikao cha serikali ya wilaya ya Kisarawe na Kamishna wa madini ukanda wa mashariki Mhandisi Ally Maganga baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika kampuni ya Rak Kaolin inayojishusisha na uchimbaji wa madini ya Kaolin na kukuta bado inaendelea na uchimbaji licha ya kuzuiwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.

Soma Pia Bodi ya maziwa yakaribisha wawekezaji

Ukaguzi uliofanywa na Mwegelo pamoja na kamati ya madini ulifanikiwa kukamata malori matatu yaliyobeba tani 100 za madini hayo zenye thamani ya Sh. 2,100,000 za kitanzania, na kuamuru kampuni kulipa faini ya ukiukaji wa maagizo ya Naibu Waziri kwa kufuata Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017. Mwegelo pia ameagiza kampuni hiyo kulipa kodi yote ambayo imekwepa.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter