Home KILIMO Vitalu nyumba kukomboa vijana

Vitalu nyumba kukomboa vijana

0 comment 98 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama amesema serikali imepanga mikakati madhubuti ya kuboresha upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini, kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa (Green House). Mhagama amesema hayo akiwa katika ziara mikoani Songea na Iringa kwa lengo la uhamasishaji na kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujenga vitalu nyumba (Green House) katika mikoa hiyo. Waziri Mhagama ameeleza kuwa serikali imeanzisha mradi huo ili kuhakikisha vijana wanafikiwa kwa kiasi kikubwa na vilevile, kuwawezesha kupata ujuzi na kujiajiri kupitia kilimo cha kisasa.

“Teknolojia hii itawawezesha vijana kulima katika eneo dogo, kupata mazao kwa wingi na kuweza kuyauza, vilevile kutumia eneo hilo kuweza kuajiri vijana wengine kwani asilimia zaidi ya 60% ya watu wanaojiajiri na kujishughulisha inatokana na mashamba”. Amefafanua Mhagama.

Mbali na hayo, Waziri huyo ameongeza kuwa vijana watafundishwa teknolojia hiyo ili waweze kuongeza thamani ya mazao yatakayozalishwa na kuagiza halmashauri zote kujipanga katika utayarishaji wa miundombinu katika maeneo hayo na kuhakikisha vijana wanatayarishwa mapema pamoja na kuanzishiwa kwa vyama vya ushirika (AMCOS) kwani wananchi wanataka kuona matunda ya mradi huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter