Home VIWANDA Mgogoro kati ya kiwanda na wakulima wapata suluhu

Mgogoro kati ya kiwanda na wakulima wapata suluhu

0 comment 140 views

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imemaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima wa chai kutoka wilayani Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate, mgogoro uliopelekea kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kufanya kazi. Waziri Majaliwa ametangaza hayo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Lushoto baada ya kutembelea kiwanda hicho.

“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja”. Amesema Majaliwa.

Katika maelezo yake, Waziri Mkuu amesema mwaka 1999, serikali iliamua kuwapatia wakulima wa chai kiwanda hicho ili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao, lengo likiwa ni kuwapatia uwezo wa kiuchumi. Kuhusu suala la madeni ya watumishi, Majaliwa ameagiza madai hayo kuorodheshwa kwa ajili ya malipo na kuwahakikisha wananchi hao kuwa, ajira zitarudi kwani serikali inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.

“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresha kilimo linafanikiwa na wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake”. Amesisitiza Majaliwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter