Home FEDHA Tucta yapinga mafao mapya ya wastaafu

Tucta yapinga mafao mapya ya wastaafu

0 comment 263 views

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Tumaini Nyamhokya amesema shirikisho hilo limepinga kanuni mpya ya kukokotoa mafao ya wastaafu iliyotolewa hivi karibuni na kudai kuwa inakandamiza wafanyakazi. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha 35 cha shirikisho hilo, Nyamhokya amesema kanuni hizo ni kandamizi na zimepokewa na wafanyakazi kwa mtizamo hasi.

Mjadala mkubwa umezuka baada ya kutangazwa kwa Kanuni mpya za Sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2014 ambazo pamoja na mambo mengine, zinaelekeza kuwa wastaafu wote watalipwa mkupuo wa asilimia 25 ya mafao wanapostaafu, huku wakilipwa asilimia 75 inayosalia kama pensheni ya kila mwezi.

“Kuunganishwa kwa mifuko ni hoja ya Tucta tangu mwaka 2004 lakini kanuni mpya ni kinyume cha mapendekezo yetu. Sisi tulitaka kanuni zibaki kuwa za mwaka 2017 ambapo kikokotoo ni 1/540 na mkupuo ni asilimia 50, huku wastani wa umri wa kuishi ukiwa ni miaka 15.5”. Amesema Nyamhokya.

Aidha, Rais huyo wa Tucta amesema kama serikali inataka usawa katika malipo ya hifadhi ya jamii, ingewapandisha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 50 waliokuwa wakipata mafao mkupo au kuongeza na kupunguza kwa kila upande ili angalau kufikia asilimia 40. Aidha, Nyamhokya amesema baada ya kikao hicho, wanatarajia kukutana na Waziri wa Kazi na kama itashindikana kufanya lolote juu ya hali iliyopo hivi sasa, shirikisho hilo litachukua hatua zaidi

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter