Home KILIMO Wakulima walilia malipo Mbeya

Wakulima walilia malipo Mbeya

0 comment 122 views

Kufuatia vyama vya ushirika kushindwa kuwapatia malipo yao kwa wakati, baadhi ya wakulima wa kahawa mkoani Mbeya wameanza kupanda miche pasipo kuwa na mbolea kutokana na kukosa fedha. Ofisa Mtendaji wa Kata ya Iwiji, Waziri Mwasenga amesema vyama hivyo vimechelewesha malipo na kupelekea wakulima kokosa fedha kwa ajili ya kununua mbolea kwa ajili ya msimu wa kupanda. Ofisa huyo ametoa wit kwa serikali kuingilia kati sintofahamu hiyo ili wakulima waweze kulipwa wanachostahili na kuendeleza kilimo chao.

“Vyama vingi vya ushirika kwa sasa vimekufa lakini vilikopa kahawa yetu na madhara yake yanaonekana, kila ukiwakuta wakulima watano mmoja pekee ndio anapanda kahawa kwa kutumia mbolea na wengine wanapanda bila mbolea”. Ameeleza Mwasenga.

Kwa upande wake, Muweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mpakani Kalinga amesema fedha za wakulima hazipiti kwa halmashauri  baada ya Bodi ya kahawa kuuza zao hilo na kuwataka wakulima kuwa watulivu wakati wakisubiri serikali ishughulikie suala hilo na kuhakikisha wanapata haki zao.

“Tunaomba mtuachie hili suala tulifuatilie ili tuone nini kilichotokea kwenye malipo ya wakulima hao, hatutegemei wakulima wakate tamaa maana kahawa ni zao muhimu sana”. Amesema Kalinga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter