Home BIASHARA Vodacom yazindua huduma mpya ya kurahisisha biashara inayoendana na mabadiliko ya kidijitali

Vodacom yazindua huduma mpya ya kurahisisha biashara inayoendana na mabadiliko ya kidijitali

0 comment 93 views

Katika jitihada za kuhakikisha biashara zinaenda sambamba na mabadiliko ya  masoko ya kisasa,kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, leo imezindua kitengo kwa ajili ya kushughulikia  huduma zinazoenda sambamba na mahitaji ya wateja wake wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-Ofisi ndogo za nyumbani (Soho’s), Wafanyabiashara  wa kati (SMEs) na Makampuni makubwa.

Lengo kuu la huduma hii ni kuwawezesha kufanya biashara kwa ufanisi zaidi, kuhimili ushindani, kujenga mtandao wa kibiashara na kuwawezesha kupata huduma zote za kurahisha biashara zao bila kuhangaika na masuala yaliyo nje ya biashara zao za msingi.

“Ulimwenguni kote kumetokea mabadiliko ya njia za kufanya biashara kutoka njia za zamani kwenda njia za kidijitali, kutumia mitandao na teknolojia za kisasa kama cloud ,tunatarajia wateja wetu kwenda sambamba na  mabadiliko haya ili kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuhimili ushindani katika masoko nasi tunaamini ni wabia wao muhimu katika kuleta ufumbuzi wa kufanikisha biashara zao”, alisema Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC.

Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, na Arjun Dhillon, Mkurugenzi wa Kitengo maalum cha Biashara wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo hicho maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam.

Makampuni makubwa kama mabenki na sekta ya umma yanatafuta ufumbuzi wa ubunifu ambao utarahisisha shughuli za uendeshaji, kuhimili ushindani na kuhakikisha mali zake ziko salama.Vodacom Tanzania PLC kampuni kinara inayoongoza kutoa huduma za ubunifu wa kidijitali inawezesha kupata huduma za utambuzi wa maeneo,huduma za kompyuta kutumia teknolojia ya kisasa ya Cloud, data MPLS,huduma za simu ambazo mpigaji hatotozwa gharama za kupiga simu na biashara kutumia  M-Pesa ili kuwezesha makampuni makubwa kufanya kazi kwa tija na ufanisi.

Msukumo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda umepelekea kuanzishwa kwa biashara ndogo na za kati ambazo uendeshaji wake kwa ufanisi unahitaji huduma za ubunifu wa kiteknolojia za kisasa ili kuzipunguzia gharama za uendeshaji

“Vodacom inayo dhamira ya kufanikisha ukuaji wa biashara nchini Tanzania kupitia ubunifu wake wa huduma za teknolojia ya kidijitali za kuwarahisishia wafanyabiashara kufanikisha malengo yao na kujiandaa kwa siku zijazo na ndio maana tumewaletea huduma hizi” alisema Bw, Hendi.

Farid Seif (wa pili kushoto) na timu ya kitengo cha biashara wakimsikiliza moja kati ya wateja wao aliehudhuria uzinduzi wa kitengo hicho maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam.

Biashara zenye ukubwa wa kati kama asasi zisizo za Kiserikali (NGO’s) ambazo zimejipanga kuendesha shughuli zake kwa njia za  kisasa na ambazo zinatoa kipaumbele kutumia teknolojia za kisasa yatafaidika na huduma  kama IoT (Internet of  Things) , SIM Manager na utumaji wa ujumbe wa maneno kwa watu wengi kwa wakati mmoja (bulk SMS).

Kwa upande wa biashara ndogo na Ofisi ndogo za nyumbani (Soho’s) zitanufaika kwa kubana matumizi na kujenga mtandao wa biashara kupitia huduma ya M-Pesa,huduma za kurahisisha biashara na utumaji wa ujumbe wa maneno kwa watu wengi kwa pamoja wataweza kubadilisha biashara zao na kuzifanya kukua zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter