Home FEDHAMIKOPO Halmashauri zinazobania mikopo zaonywa

Halmashauri zinazobania mikopo zaonywa

0 comment 110 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ameagiza wakurugenzi katika Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha mikopo maalum inayotolewa kwa ajili ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inatolewa kama Sheria inavyoelekeza.

Waziri Jafo amewaambia waandishi wa habari kuwa Halmashauri zitakazoshindwa kufanya hivyo zitachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria na kuongeza kuwa, japokuwa Sheria ipo, mchakato wa utoaji hiyo kwa baadhi ya Halmashauri umeendelea kusuasua.

“Hivi sasa hakuna kisingizio chochote katika utekelezaji wa Sheria hii kwani serikali imeshatoa kanuni, zinazoongoza utoaji wa mikopo hiyo na kanuni hizo zimetangazwa katika gazeti la serikali toleo Na. 141 la tarehe 5 April, 2019 kwa GN. Na. 286 la mwaka 2019 kwa hiyo Mkurugenzi atakayeshindwa kutekeleza kwa ufanisi atachukuliwa hatua”. Amesema Jafo.

Waziri huyo ametaja baadhi ya Halmashauri 23 ambazo utekelezaji wa utoaji mikopo hiyo umekuwa sio wa kuridhisha kuwa ni Nsimbo, Nyasa, Busega, Kondoa Dc, Namtumbo, Kasulu Dc, Bariadi Dc, Msalala, Mbulu Tc, Njombe Dc, Kongwa Dc, Musoma Mc, Sumbawanga Dc, Kondoa Tc, Uvinza Dc, Ilala Mc, Lindi Dc, Mpwapwa Dc, Bahi Dc, Chamwino Dc, Momba Dc, Temeke Mc, Mbulu Dc na Lindi Mc.

“Mkurugenzi yeyote atakayeshindwa kutoa fedha kwa vikundi kama ilivyoanishwa hapaswi kumlaumu mtu yeyote kwa sababu atachukuliwa hatua kama ilivyoelekezwa kwenye Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi”. Amesisitiza.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter