Home BENKI Unapochagua benki zingatia haya

Unapochagua benki zingatia haya

0 comment 115 views

Unapochagua benki, ni muhimu kupata bidhaa, huduma, na viwango ambavyo hukutana na mahitaji yako. Unapotathmini benki kubwa dhidi ya benki ndogo pamoja na taasisi za mikopo unaweza kujiuliza kama ukubwa wa taasisi ni muhimu. Kwa kiwango fulani ni muhimu lakini ifahamike kuwa benki ndogo na kubwa zote zinaweza kutoa huduma muhimu kama kuangalia na kuhifadhi fedha katika akaunti.

Ni muhimu kuzingatia haya:

  • Urahisi

Chagua benki ambayo ni rahisi kufanya nayo kazi kulingana na masharti yaliyopo. Kama unataka kufanya masuala binafsi ya kibenki basi jua kuwa kuna taasisi ambazo zina uwezo wa juu zaidi kuliko zilizopo katika eneo lako.

  • Gharama

Mara nyingi malipo hupungua katika taasisi ndogo, lakini sio wakati wote. Tambua mahitaji yako ya benki na ulinganishe ada kwa huduma unayohitaji.

  • Huduma

Taasisi ndogo muda mwingine hutoa huduma na bidhaa kubwa za kushangaza licha ya hivyo muda mwingine huduma na bidhaa kutoka katika benki kubwa huhitajika.

  • Jumuiya

Kutumia benki katika jumuiya yako kutasaidia kukuza uchumi wa ndani na kurahisisha uzoefu kuhusu masuala ya benki lakini unatakiwa kujua kila kitu kina faida na hasara zake.

Tofauti:

Kulingana na mahitaji yako ni rahisi kufanya maamuzi benki ipi inakufaa. Kwa mfano kama unahitaji kupata huduma ya benki kwa mambo binafsi kila baada ya muda mchache basi ni afadhali kutumia benki zenye matawi mengi katika sehemu mbalimbali kama vile CRDB na NMB. Na ikiwa unataka kuhifadhi fedha na kufanya miamala mikubwa ya kifedha si vibaya kutumia benki ambazo mara nyingi hupatikana zaidi katika miji mikubwa. Baadhi ya benki hizo ni kama Stanbic, Diamond Trust na Commercial Bank of Africa (CBA). Jambo la muhimu ni kuangalia kama unaweza kumudu vigezo na masharti na kama utanufaika zaidi kwa kutumia benki hiyo.

Sio rahisi sana kupata huduma kwa wateja katika benki kubwa kama ilivyo katika benki/taasisi ndogo za fedha. Kwa mfano upo mkoani na unahitaji huduma katika benki ambayo ipo maeneo machache, kwa namna moja au nyingine itakulazimu kutumia muda na hata gharama kubwa kwenye usafiri ili kupata nafasi ya kutatua tatizo lako. Lakini kwa benki kama CRDB ni rahisi zaidi kwa sababu mteja hutakiwa kufika katika tawi lililopo karibu yake na kutatua tatizo lake kwa muda mfupi.

Gharama hutofautiana katika benki ndogo na kubwa. Benki ndogo hutoza ada za kawaida kufanya miamala ya benki huku benki kubwa zinaweza kutoza zaidi au kutotoza ada kabisa.

Kuhusu ushindani katika ada za viwango, katika benki za ndani huwa wanajitahidi sana kuwavutia wateja ikiwa ni pamoja na kuweka viwango vya kuvutia kwa mfano kuangalia kiasi cha fedha ni bure na utalipia pale utakapohitaji kutumiwa habari fupi kielektroniki. Pia katika masuala ya mikopo na viwango vya kuweka akiba kuna ushindani baina ya benki kubwa na ndogo. Ieleweke kuwa viwango vya akiba vinaweza kuwa vikubwa katika benki lakini hii haitakiwi kukuogopesha kuwa na akaunti katika taasisi husika.

Unaweza usiwe na uhakika wa kupata mkopo kutoka katika benki kubwa lakini benki ndogo zimejikita katika kuhakikisha unapata mkopo kwa ajili ya biashara, kilimo, mali n.k katika eneo husika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter