Home AJIRA Biteko ataka wabunifu wazawa kuinuliwa, kunadiwa Kimataifa

Biteko ataka wabunifu wazawa kuinuliwa, kunadiwa Kimataifa

0 comment 38 views

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na jitihada za kuwainua wabunifu wawekezaji nchini, bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwawezesha wabunifu wetu kukua zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Dkt. Biteko amesema hayo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Uwekezaji wa Kampuni Bunifu (STARTUPs)

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.

Amesema kuwa Tanzania imerekebisha mifumo mingi ili kuwezesha ubunifu na uwekezaji wa moja kwa moja nchini kuleta maendeleo, suala ambalo tumeona likifanikiwa na kwahiyo linahitaji kupaliliwa na kuungwa mkono kwa matokeo chanya.

“Nimewasikiliza wanakongamano na kupitia majadiliano haya ni wazi kwamba bado kuna namna ya kuboresha zaidi mifumo yetu ya usimamizi na utawala ili kuhakikisha Wabunifu wanapata nafasi nzuri zaidi.

Tunatamani kuona Watanzania wanashiriki katika kukuza uchumi wa nchi yao na pengine kuazimwa katika nchi nyingine,” amesema Dkt. Biteko

Amesema wapo baadhi ya Watanzania wanaofanya shughuli zao nje ya nchi ambao wanaiwakilisha vema Tanzania kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia misingi iliyowekwa katika nchi hizo na hivyo kuwataka wabunifu wawekezaji kuiga mfano huo.

Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan yako wazi na kwa nyakati mbalimbali amekuwa akijipambanua kuhusu uwezeshaji wa makundi mbalimbali wakiwemo wabunifu wawekezaji.

“Kwa kutekeleza maono ya Rais, ni muhimu kuwasikiliza, kuwaamini na kufanyia kazi maoni na bunifu zao ili kuboresha mazingira yatakayo wawezesha kutekeleza Bunifu zao na kupata fursa ndani na nje ya nchi”.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter