Home BENKI BoT yamgusa Shein, atoa neno

BoT yamgusa Shein, atoa neno

0 comment 106 views

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imepongezwa kwa utendaji bora wa kazi na jitihada zake za kuhakikisha uchumi wa nchi unazidi kustawi kwa manufaa na maslahi ya wananchi. Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ikulu visiwani Zanzibar alipofanya mazungumzo na viongozi wa benki hiyo akiwemo Gavana wake, Prof. Frolens Luoga.

Dkt. Shein Amesema kuwa juhudi kubwa zilizochukuliwa na BoT zimeonyesha nguvu kubwa katika kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo na kuwataka viongozi hao kuhakikisha BoT inachukua hatua kadhaa kuhakikisha kunakuwa na mzunguko wa fedha, ili kuwasaidia wananchi na taifa kwa ujumla.

“Uchumi wa Zanzibar na ule wa bara umeimarika , miongoni mwa wanaochangia jambo hilo ni BoT”. Amesema Dk. Shein.

Soma Pia Riba mpya za Bot kuanza kutumika leo

Aidha Dk. Shein ameitaka benki kuu kujikita katika kusimamia sekta za uchumi na maendeleo ikiwemo sekta ya utalii visiwani humo ili kuwanufaisha wananchi ambao ni walengwa wakubwa katika uanzishaji wa benki hiyo.

Kwa upande wake, Gavana Luoga amesema matokeo mazuri ya utendaji kazi wa BoT umetokana na kutambua dhamana waliyopewa na wananchi kusimamia benki hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia sera za fedha, kuhakikisha utulivu wa fedha na uchumi usiotetereka, mambo ambayo yamekuwa yakitekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Soma Pia Majukumu ya BoT katika kukuza uchumi

Aidha Prof. Luoga amewatoa hofu wananchi kuwa BoT itaendelea kuhakikisha usimamizi bora wa fedha ili kuhakikisha zinafanya kazi zake kwa ubora kwa ajili ya kuwafikia wananchi, huku akiongeza kuwa moja ya mipango ya benki hiyo ni kujikita zaidi katika kuboresha huduma zake maeneo ya vijijini ili kuwaletea wananchi maendeleo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter