Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda amesema benki hiyo imezindua rasmi kampeni inayofahamika kama “Deposit Utokelezee na Exim” yenye lengo la kutoa hamasa kwa watanzania kujenga mazoea ya kuweka akiba zaidi. Kampeni hiyo inawawezesha wateja kupata viwango vya riba hadi asilimia 10.5 watakapofungua akaunti ya amana maalum au kuweka kwenye akaunti zao za amana maalum kiasi kisichopungua Sh. 50 milioni kabla ya Desemba 31 mwaka huu.
“Kampeni hii inalenga kukuza utamaduni kwa kuzingatia viwango vya ushindani tunavyowasilisha kupitia kampeni hii, wateja wetu watakuwa na uwezo wa kunufaika na riba ya hadi asilimia 10.5 kwenye amana zao. Kama benki tunaahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wateja wetu ili kuhakikisha wanakuwa na ustawi mzuri sasa na hata baadae. Kupitia akaunti zetu za muda maalum mteja anaweza kuongeza kiasi kikubwa cha pesa, huku akiwa na uhuru wa kuchagua aina ya muda anaotaka. Tunaamini kwamba kesho yako bora inaanza leo”. Ameeleza Kaganda.
Kampeni hiyo ni muendelezo wa Benki ya Exim katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama “Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho” ambao unaendana na mwelekeo wa benki hiyo.