Home BENKI Riba ya Benki Kuu kusalia asilimia sita

Riba ya Benki Kuu kusalia asilimia sita

0 comment 121 views

Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema Riba ya Benki Kuu (CBR) kwa kwa robo ya mwisho wa mwaka 2024 itabaki kuwa asilimia sita.

Gavana wa BoT Emmanuel Tutuba ameeleza hayo Oktoba 03, 2024 jijini Dodoma kuwa uamuzi huo umeafikiwa kutokana na matarajio ya mfumuko wa bei kuendelea kuwa chini ya lengo la nchi la asilimia 5.

Tangu robo ya pili ya mwaka 2024 kiwango hicho cha riba kimebakia kuwa asilimia sitabaada ya kuongezwa kidogo mapema nwezi Aprili.

Amebainisha kuwa “kamati pia inatarajia uchumi kuendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha, sambamba na kuimarika kwa mazingira ya kiuchumi duniani.”

Kamati hiyo iliyoketi Oktoba 2, 2024 inatarajiwa kuwa uchumi wa dunia utaendelea kukua sambamba na kuimarika kwa mazingira ya upatikanaji fedha.

Gavana Tutuba amesema kuwa kamati ilibaini kuwa utekelezaji wa sera ya fedha ulifanikiwa kuhakikisha mfumuko wa bei unabaki ndani ya lengo la asilimia 5.

Mfumuko wa bei Tanzania uliorekidiwa mwezi Julai kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umeendelea kuwa imara ukiwa kati ya asilimia 3.0 na 3.2 ndani mwaka mmoja.

Aidha katika mwaka unaoishia Agosti 2024, mfumuko wa bei uliongozeka kidogo hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 3.0.

Amesema “katika robo ya kwanza ya mwaka 2024, uchumi ulikuwa kwa asilimia 5.6 huku shughuli za ujenzi, kilimo, fedha, bima na usafirishaji vikichangia kwa kiwango kikubwa katika ukuaji huu.”

Kwa mujibu wa viashiria vy awali, amesema uchumi unakadiriwa kukua kwa 5.8% na 5.6% katika robo ya pili nay a tatu ya mwaka 2024, mtawalia na unatarajiwa kuendelea kukua katika viwango hivyo katika robo ya mwisho wa mwaka.

Ukuaji huo unatarajiwa kuchangiwa zaidi na kuendelea kuimarika kwa mazingira ya kiuchumi nchini kutokana na maboresho katika uwekezaji na biashara na kuboreka kwa uchumi wa dunia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter