Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imetoa ofa ya kujenga masoko ya kisasa kwaajili ya machinga kwenye Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amefanya kikao baina ya na viongozi mbalimbali kujadili suala hilo.
Akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, RC Makalla amesema Benki hiyo imeamua kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita kuboresha mazingira ya machinga walioamua kuitikia wito wa Serikali kufanya biashara kwenye maeneo waliyopangwa.
Ili kufanikisha mpango huo unaokwenda kuchochea biashara, RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kumkabidhi taarifa kamili inayoainisha wapi masoko hayo yajengwe, michoro na gharama halisi kabla ya Ijumaa ili awasilishe kwa Bank hiyo kwaajili ya utekelezaji.
Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TANROAD, TARURA, DAWASA, TANESCO, LATRA kuhakikisha kuanza kwa maandalizi ya kuhakikisha Maeneo yanapojengwa masoko hayo yanakuwa na huduma zote muhimu ili kuchochea biashara.
Patricia Laverley, meneja wa ADB tawi la Tanzania amesema kuwa Benki hiyo ipo tayari kutekeleza Ujenzi wa masoko hayo kwakuwa wameguswa na jitiada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wafanyabiashara wanaendesha biashara kwenye maeneo sahihi na Bora.