Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Vitambulisho 11,000 kuwafikia wajasiriamali Ikungi

Vitambulisho 11,000 kuwafikia wajasiriamali Ikungi

0 comment 93 views

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu amesema wilaya hiyo imejipanga kukamilisha ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo 11,000 hadi kufikia Machi 28 mwaka huu. Mtaturu ameeleza kuwa wanatarajia kufanikisha lengo hilo kwa kushusa ugawaji wa vitambulisho hivyo hadi kwenye ngazi ya watendaji wa kata ili kuwafikia na kuwatambua wafanyabiashara kwa urahisi.

“Tulichofanya tumeshusha vitambulisho kwa watendaji wa kata ili kurahisisha zoezi hilo na kuwatambua kwa haraka, hapa Ikungi tuna kata 28, kila Mtendaji tumempa vitambulisho mia moja ingawa wengine tumewapa mia mbili kulingana na eneo lake”. Amesema Mkuu huyo.

Pamoja na hayo, Mtaturu ameweka wazi kuwa changamoto kubwa hadi sasa ni maelekezo waliyopatiwa awali ya kutoa vitambulisho kwa wale wasio na namba ya mlipa kodi (TIN), japokuwa wengine walikuwa na namba hizo kwa ajili ya kumiliki pikipiki na kupata mikopo, na sio kulipa kodi. Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kijitokeza na kuchukua vitambulisho ambavyo gharama yake ni Sh. 20,000 tu.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter