Home BIASHARA Bomba la mafuta kunufaisha watanzania

Bomba la mafuta kunufaisha watanzania

0 comment 124 views
Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu amesema baraza hilo linatarajia kuwezesha wananchi kupata fursa mbalimbali kutokana na ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta.

Mradi huo utakaoanzia Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga uliwekwa jiwe la msingi na Rais John Magufuli pamoja na Rais Yoweri Museveni unategemea kuzalisha ajira mbalimbali katika mikoa 8 wilaya 24 na vijiji 184 nchini, ambapo mwenyekiti huyo amewashauri vijana nchini kuchangamkia nafasi hizo.

Ajira 10,000 zitatolewa kipindi cha mradi huo, na pindi utakapomalizika, ajira za kudumu 1,000 zitatolewa. Hivyo basi taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo VETA zimeshauriwa kuandaa vijana wanaokidhi vigezo ili kutumia fursa hizo.

Baraza hilo linashirikiana na mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Singida , Tabora, Tanga, Manyara na Dodoma ambapo bomba hilo litapita. Baraza hilo limejipanga kuwanufaisha watanzania kupitia mradi huu ambapo baadhi ya ajira zitakazotolewa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, ulinzi na uuzaji wa bidhaa za ujenzi pamoja na huduma za chakula. Taarifa zaidi juu ya fursa hizi zitapatikana katika ofisi za halmashauri pamoja na tovuti ya NEEC.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter