• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, September 24, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Umaskini usiwe kigezo cha kukosa elimu

Patricia Richard by Patricia Richard
May 16, 2018
in MIKOPO
0
Share on FacebookShare on Twitter

Ili kufanikisha masomo yao ya elimu ya juu, wanafunzi wengi hutegemea kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Kutokana na hali ya chini ya kiuchumi, watanzania wengi huchukulia bodi hii kama suluhisho pekee ili kufanikiwa kumudu gharama mbalimbali zinazokuja baada ya kuanza masomo yao vyuoni. Lakini sio wote wamekuwa wakibahatika na kufadhiliwa. Wengi wameendelea kuachwa nyuma katika hili hivyo kushindwa kujiendeleza kielimu hali ambayo inawaweka katika mazingira magumu kimaisha.

Mfumo wetu wa elimu umekuwa kikwazo kwa vijana wengi wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa za elimu ya juu. Kutokana na masharti ambayo siyo rafiki kwa wengi, kundi kubwa la vijana wameendelea kukosa haki yao ya msingi ya elimu kwa sababu tu hawana uwezo kifedha. lakini kwanini mwanafunzi akose elimu eti kisa ni maskini? Vipi kuhusu mchango wake katika kujenga Tanzania mpya ya viwanda? Miaka mitano ijayo vijana hawa watakuwa katika hali gani kiuchumi? Kwanini basi kusiwe na suluhisho mbadala la kusawaidia watu hawa?

Kila mtu anayo haki ya kupata elimu bila kujali uwezo alionao kiuchumi. Kwa kuwanyima fursa za elimu vijana, wataalamu tutawapata wapi? Vijana hawa watajikwamua vipi na hali ngumu ya maisha kama hata mikopo ya elimu ni mtihani? Wabaki tu mitaani bila kazi wala ajira kwa sababu tu walishindwa kugharamia elimu yao ya juu?

ADVERTISEMENT

Mwezi Agosti mwaka jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru alisema bodi hiyo imejipanga kutoa mikopo kwa wanafunzi zaidi ya 30,000 kwa mwaka wa masomo 2107/2018 huku kati yao asilimia 40 wakiwa wanafunzi wa masomo ya afya, sayansi ya elimu na hesabu. Mara nyingi wengi wanaojikita katika masomo ya sayansi hujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kupata mikopo kutoka katika bodi hiyo. Lakini kwa mwanafunzi asiye na historia na masomo ya sayansi nafasi yake ya kupata mkopo ikoje? Fani anayotegemea kusoma haina thamani kama zilivyo hizo nyingine? Hana mchango wowote katika kujenga taifa?

Ni kweli kwamba tasnia zinazotokana na masomo ya sayansi hazichaguliwi na wanafunzi wengi hivyo serikali kupitia bodi ya mikopo huweka mazingira mazuri kwa wachache wenye dhamira ya kusoma masomo hayo na njia moja ya kufanya hivyo ni kuwapatia mikopo. Lakini katika kufanya hivyo ni vizuri kama wanafunzi wengine hawatasahaulika. Kuwe na utaratibu ambao utawawezesha na wao kupata mikopo hiyo ili wapate elimu. Kila mmmoja wetu ana haki ya kujiendeleza kielimu hivyo wanafunzi wote kwa pamoja wawezeshwe katika hili ili wapate fursa ya kutimiza ndoto zao.

Tags: elimu ya juuheslbmikopo
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post

Serikali iimarishe ngazi hizi muhimu za maendeleo

Discussion about this post

Habari Mpya

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

September 14, 2023

Benki ya Exim yajikita uwazi shughuli za bima

September 14, 2023
Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande.

Tanzania yapiga hatua utakatishaji fedha

September 12, 2023
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Picha| Ikulu

Tutawaunganisha wakulima na soko: Rais Samia

September 11, 2023

Mbaazi yaleta neema kwa wakulima 2023

September 7, 2023

Bei za mafuta zapanda tena Tz

September 6, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

by Pesatu Reporter
September 14, 2023
0

Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa asali barani Afrika na inashika nafasi ya 14 dunia. Ethiopia, ndio nchi...

Benki ya Exim yajikita uwazi shughuli za bima

by Pesatu Reporter
September 14, 2023
0

Benki ya Exim imezindua ushirikiano wa kimkakati na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na kufanya mafunzo ya...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In