Home BIASHARA Forex yapamba moto

Forex yapamba moto

0 comments 184 views

Biashara ya Forex inakuja kwa kasi hapa Tanzania na Afrika Mashariki hasa kwa vijana ambao wamekuwa wakipeana habari kupitia mitandao ya kijamii. Biashara hii imekuwepo miaka mingi hususani katika nchi zilizoendelea. Kwa hapa nyumbani, imekuwa ngumu kuwahamasisha watanzania kufanya biashara hii kwa sababu wengi wamekuwa wakihofia kutapeliwa. Kujihami si jambo baya na katika kila kitu kuna mazuri na mabaya.

Yafuatayo ni mambo kadhaa kuhusu biashara hii yatakayokusaidia kupata uelewa zaidi na kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi kama unafikiria kujiunga.

Forex ni nini?

Forex ni neno la kiingereza linalounganisha maneno mawili, FOREIGN (kigeni)  na EXCHANGE (kubadilisha) ambayo kwa pamoja zinamaanisha ubadilishaji wa fedha za kigeni.

Biashara ya Forex ni nini?

Ni mfumo ambao upo dunia nzima. Unamuwezesha mtu yeyote kununua fedha za nchi nyingine na kutokana na sababu mbalimbali (nitazitaja hapo chini). Kushuka au kupanda kwa thamani ya fedha hizo kunaweza kumletea mtu huyo faida au hasara.

Mfano mtu akiwa na Dola 20 halafu anataka kuzibadilisha kuwa shilingi za kitanzania atapata shilingi 46,304.00. Hapo inamaanisha mwenye Dola atapata faida na aliyeuza Shilingi hatopata faida.

Unaweza nunua fedha za nchi nyingine ambazo unajua baada ya muda fulani thamani yake itapanda. Unaweza ukawa sawa kuhusu kupanda au kushuka kwa thamani ya sarafu hiyo na ndio maana watu wengi husema biashara hii ni risky (hatari).

Jambo zuri kuhusu biashara hii ni kwamba mtu yeyote mwenye mtaji anaweza kuifanya. Inaweza kufanyika kielektroniki kwa kutumia simu au kompyuta, hivyo ni rahisi kufanya Forex na kuendelea na shughuli nyingine.

Kabla hujafanya maamuzi unatakiwa kuzingatia malengo yako ya kufanya biashara hii, uzoefu ulionao na utayari wa kufaidika au kupata hasara. Anayefanya biashara hii kielektroni huingiza fedha zake kwenye kampuni za madalali ambao wao hukutanisha wafanyabiashara kutoka pande zote za dunia. Makampuni hayo huwa na kiingilio/mtaji. Baada ya kuweka, fedha hizo huingizwa katika soko la Forex  na mfanyabiashara huyo huanza kupata faida moja kwa moja. Kutokana na makubaliano baina yake na kampuni, mfanyabiashara ataingiziwa fedha zake kwenye simu au akaunti yake ya benki. Mfanyabiashara yupo huru kutoa fedha zake zote kwenye soko la Forex muda wowote anaotaka baada ya kufanya mawasiliano na wahusika.

Viashiria hivi husaidia kujua kama thamani ya fedha inashuka au kupanda ikilinganishwa na fedha za nchi nyingine:

  1. Mfumuko wa bei. Kama nchi ambazo tunafanya nao biashara kwa mfano Marekani thamani ya Dola ikipanda,  moja kwa moja fedha yetu inapoteza thamani. Hivyo mtu hashauriwi kununua Shilingi yetu, na la muhimu zaidi ni kwamba kila senti ina thamani katika biashara hii. Mfanyabiashara anapaswa kuwa makini.
  2. Kabla hujafanya biashara ya Forex unatakiwa kuangalia uingizaji na utoaji wa bidhaa na huduma wa nchi unayotaka kununua au kuuza fedha. Kama nchi hiyo inaagiza kuliko inavyoingiza basi moja kwa moja thamani ya fedha inakuwa chini kwa sababu presha ya Dola inakuwa kubwa na Shilingi inashuka thamani.
  3. Suala la amani ya nchi husika ni muhimu. Kama nchi ipo vitani ni dhahiri kwamba thamani ya fedha ipo chini hivyo kama unataka unufaike baadae unaweza kununua fedha za nchi hiyo na kuziuza baadae thamani yake itakapopanda.
  4. Uchumi ukiwa unakuwa na thamani ya fedha pia inakuwa hivyo ukibaini hali ya uchumi katika nchi unayotaka kununua fedha inakuwa rahisi kufanya maamuzi sahihi.

Jambo la msingi na la muhimu ni kuwa mfuatiliaji wa habari ili kujua yanayojiri duniani. Hii itakusaidia kufanya uamuzi wa uhakika pale unataka kununua au kuuza fedha zako.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!