Home BIASHARA Pima wazo lako la biashara hapa

Pima wazo lako la biashara hapa

0 comment 105 views

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakianzisha biashara ambazo hushindwa kustahimili ushindani uliopo sokoni.  Hii ni kutokana na kwamba, mawazo yao hayakufanyiwa tathmini ya ubora hivyo biashara ilikosa muelekeo mzuri tangu mwanzo. Kabla ya kuwekeza kwenye biashara, ni muhimu kuwa na wazo bora la biashara ambalo litakuwa muongozo wako.

Je, unajuaje wazo lako ni bora?

Ikiwa wewe ni mfanyabiashara, unaweza kutathmini ubora wa wazo lako kabla ya kuanzisha rasmi biashara kwa kujiuliza maswali haya muhimu:

  • WAZO LAKO LINATATUA TATIZO?

Endapo wazo lako ni suluhisho kwa tatizo fulani ambalo litafanya maisha ya watu wanaokuzunguka kuwa rahisi, basi biashara unayofikiria ni sahihi. Kumbuka, sio lazima ufikirie kitu ambacho tayari hakipo sokoni. Unachotakiwa kuhakikisha ni kwamba, wewe unatoa huduma bora zaidi kuliko wengine ili kuwavuta wateja na kuwa na uhakika wa soko. Kama wazo lako halifanyi hivi, basi tafakari tena kwa makini na fanya maboresho kabla ya kuanzisha biashara.

  • WAZO LAKO LINAKUA?

Ili kuwa na biashara yenye mafanikio, wazo lako linahitaji kuwa na mbinu ambazo zinaonyesha namna gani biashara yako itakua na kuwavutia watu wengi zaidi. Hivyo basi, kutokana na wazo lako, unaona uwezekano wa biashara au huduma yako kuwashawishi watu kuitumia? Wazo bora la biashara linatakiwa kuzingatia suala la ukuaji. Endapo kipengele hiki kitakosekana, biashara itakayoanzishwa itakuwa kwenye hatari kubwa ya kufa.

  • UHITAJI WA WATU UKO VIPI?

Ni wazi kwamba ili uuze bidhaa, ni lazima watu wawe na uhitaji nayo. Inatakiwa kuwa kitu ambacho watu wanahitaji katika maisha yao ya kila siku. Ni vizuri kujadili wazo lako na ndugu pamoja na marafiki wa karibu (mara nyingi hawa ndio hugeuka kuwa wateja wazuri) na ikitokea wameuliza ni lini wanaweza kupata bidhaa/huduma yako, basi upo katika nafasi nzuri. Hakikisha unafanya kitu ambacho uhitaji wake ni mkubwa ili kuwa na soko la uhakika.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter