Home BIASHARA TRA kutoza faini kwa wasiodai risiti

TRA kutoza faini kwa wasiodai risiti

0 comment 77 views

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kagera Adam Ntoga ametangaza kuwa mamlaka hiyo itaanza kuwachukulia hatua wananchi ambao hawatakuwa na risiti baada ya kufanya manunuzi, lengo likiwa ni kuwakumbusha kudai risiti kila wanaponunua mahitaji yao. Ntoga amesema kuwa hatua hiyo itenda sambamba na ile ya kuwafuatilia na kuwakamata kwa mujibu wa sheria wafanyabishara wasiotoa risiti kwa wateja pamoja na wale wanaotoa risiti inayoonyesha kiasi cha fedha kisichoendana na thamani halisi ya bidhaa.

“Wananchi kwa ujumla hawana utamaduni wa kudai risiti wanaponunua bidhaa, tunajitahidi kuwaelimisha mara kwa mara, lakini hili bado ni tatizo, ndiyo maana tumekuja na mkakati wa kumuadhibu mwananchi ili aone umuhimu wa kudai risiti kila anaponunua bidhaa”. Ameeleza Meneja huyo.

Ntoga amesema japokuwa bado kuna wafanyabishara wasio waaminifu ambao bado wanaendelea kufanya biashara ya magendo, mamlaka hiyo inaendelea kufanya kila jitihada ili kuhakikisha biashara hiyo inafikia kikomo. Aidha, licha ya changamoto zinazojitokeza, makusanyo ya mapato yameongezeka na kufikia Sh.12.5 bilioni katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu.

“Lengo la makusanyo ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 inayoanzia Julai hadi Septemba lilikuwa ni zaidi ya Sh. 12.1 bilioni, lakini tumekusanya zaidi ya Sh. 12.5 bilioni kwa hiyo tumevuka lengo”. Amesema Ntoga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter