Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji watakiwa kuchangamkia fursa

Wawekezaji watakiwa kuchangamkia fursa

0 comment 121 views

Kufuatia lengo la viwanda la 2025 nchini, wawekezaji wamehimizwa kuchangamkia fursa za uwekezaji ili lengo hilo liweze kutimia. Makamu wa Rais wa Chama cha Biashara,viwanda na Kilimo (TCCIA) Octavian Mshiu amesema kuwa Tanzania ina soko kubwa la uwekezaji na fursa nyingi za kibiashara na hivyo wawekezaji hao wanakaribishwa kufanya utafiti ambao utapelekea kufanya uwekezaji.

Akizunguma wakati wa ufunguzi wa  soko la 14 la biashara Tanzania Makamu huyo ameeleza kuwa ili serikali iweze kutimiza lengo lake linawategemea wawekezaji wa nje pia kuwekeza na kwamba maonyesho hayo ni moja ya kujenga uhusiano mzuri baina ya serikali na nchi kama India.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kampuni ya CTI Subhash Patel, amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na kuwataka kuja kuwekeza bila kusita.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu anayewakilisha India nchini, Sandeep Arya amesema kuwa India na Tanzania zitaendelea kuwa na ushirikiano kwa muda mrefu na hivyo kuwataka watu wenye makampuni nchini kutoa ushirikiano na wawekezaji wa nje hususani watokao bara la Asia ili kufaidika kwa mfano kwenye sekta ya kilimo. Pia ameongeza kuwa biashara zitakazofanyika kwa usawa zitaongeza mafanikio kwa wafanyabiashara nchini na nje na hivyo kupata fursa zaidi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter