Home BIASHARA Wezi wa mafuta wapewa onyo

Wezi wa mafuta wapewa onyo

0 comment 101 views

Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoani Dodoma Luppy Shirima ametoa onyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta walio na tabia ya kuwaibia wateja kwa kukorofisha pampu ili kutoa majibu tofauti na kupunguza ujazo halisi wa mafuta. Shirima amesema hayo wakati wa mahojiano kuhusu kukithiri kwa vitendo hivyo kwa watumiaji wa huduma hiyo vinavyofanywa kwa makusudi na wauzaji.

Meneja huyo ameeleza kuwa japokuwa kumekuwa na jitihada mbalimbali za kuzuia wizi huo, baadhi ya wafanyakazi wa vituo hivyo, wamekuwa wakizikorofisha na kuzirudisha vilevile. Licha ya kuweka mitego na kufanya ukaguzi wa kushutukiza katika vituo vya mafuta, biashara hiyo haramu sasa imeanza tena katika maeneo mbalimbali hata kufikia mafuta hayo kuuzwa katika chupa ndogo za maji.

Uuzaji wa mafuta hayo kiholela unaweza kuleta hatari kubwa endapo ajali ya moto ikitokea na WMA imejipanga kushirikiana na vyombo husika ili kuwashughulikia wale wanaojihususha na biashara hiyo. Aidha, adhabu inayotolewa kwa kosa hilo ni kulipa faini kuanzia Sh. 100,000 hadi Sh. 20 milioni kulingana na ukubwa wa kosa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter