Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Ineke Bussemaker amesema kutokana na faida ya benki hiyo kushuka mwaka jana, gawio la wanahisa limeshuka kutoka Sh. 104 mpaka Sh. 64. Bussemaker amedai kuwa hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ugumu wa biashara pamoja na ongezeko la mikopo chechefu.
Mbali na kushuka kwa gawio la wanahisa, hesabu za benki hiyo zinaonyesha kuwa faida nayo imepungua kutoka Sh. 154 bilioni mwaka jana hadi Sh. 93 bilioni mwaka jana. Bussemaker amesema faida ya benki hiyo imepungua kwa asilimia 39 lakini wamejipanga kuipandisha mwaka huu na hadi kufikia sasa, hesabu zinawapa matumaini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Prof. Joseph Semboja amesema taasisi nyingi zilipunguza biashara na hata kufunga maduka lakini benki hiyo ilipambana na kupata faida.