Home FEDHAMIKOPO Meya aomba wananchi kujitokeza kukopa

Meya aomba wananchi kujitokeza kukopa

0 comment 111 views

Naibu Meya wa Manispaa ya Tabora Yahaya Muhamali amewataka wananchi wanaolengwa na mkopo wa asilimia 10 kujitokeza kwa wingi na kuomba mikopo hiyo kwani fedha kwa ajili ya kukopesha zipo. Muhamali amesema hayo wakati wa mkutano wa hadhara ambapo amewataka wananchi, wafanyabiashara  na wajasiriamali wa mkoa huo kujitokeza katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Katika maelezo yake, Naibu Meya huyo amesema Manispaa imetenga Sh.30 Milioni kwa ajili ya malengo ya kukopesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu lakini hadi sasa wito wa vikundi hivyo kukopa fedha hizo umekuwa mdogo.

Muhamali ametoa wito kwa wanawake, vijana na watu walio na ulemavu kujiunga katika makundi na kujisajili kwa ajili kufika Manispaa ya Tabora na kupatiwa taratibu za kuomba mkopo ambao utawasaidia kuendesha shughuli zao na kupiga vita umaskini. Naibu Meya huyo pia ametaja moja ya sababu wa watu kuogopa kwenda kukopa ni historia ya baadhi ya taasisi ambazo zinaendesha biashara ya kukopesha wananchi kwa kuwadai riba kubwa hali iliyopelekea watu kufilisika.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter