Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Uhalifu wa kodi Afrika Mashariki kudhibitiwa

Uhalifu wa kodi Afrika Mashariki kudhibitiwa

0 comment 90 views

Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Salim Kessi amezitaka mamlaka za mapato Afrika ya Mashariki chini ya kitengo cha wapelelezi wa kodi kuchukua hatua za haraka, ikiwa ni pamoja na kuandaa mchakato wa kuwajengea uwezo wapelelezi wa kodi sambamba na mfumo wa kisheria ili kuwasaidia kupambana na uhalifu.

Kessi ametoa mapendekezo hayo alipokuwa akifungua mkutano wa wajumbe wa kamati ya ufundi ya makamishna wa upelelezi wa kodi wa mamlaka za mapato ukanda wa Afrika Mashariki unaofanyika visiwani Zanzibar. Kamishna huyo amezitaka mamlaka hizo kufanya mchakato huo mapema kwa ajili ya kusaidia kupunguza uhalifu wa kodi ili kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kuwa kadri mamlaka hizo zitakavyochelewa ndivyo zitakavyozidi kupoteza mapato.

“Tunataka mchakato huu umalizike mapema ili tuweze kupambana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi kwani kadri tunavyochelewa ndivyo wahalifu wanaendelea kusababisha upotevu wa kodi kwa mamlaka zetu za mapato” . Amesema Kessi.

Aidha Kessi amesema kuwa siku nne za mkutano huo zimeambatana na uwasilishaji wa wazo hilo ili kuweza kuliwasilisha katika kikao cha makamishna wa upelelezi wa kodi wa Afrika Mashariki ili kupambana na kudhibiti uhalifu wa kodi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter