Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema hadi kufikia tarehe 14 Desemba mwaka huu, jumla ya wakulima 130,163 wamelipwa kiasi cha Sh. 133,259,933.855. Waziri Hasunga ametoa takwimu hizo wakati akizungumza katika mkutano wa wabanguaji uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kueleza kuwa, mkoani humo, wananchi ambao wameshalipwa wanafikia 77,055 huku jumla ya fedha iliyolipwa ikiwa ni Sh. 80,098,982,060 bilioni.
Kwa mkoa wa Lindi, wakulima waliolipwa hadi sasa ni 41,564 ikiwa wamepatiwa Sh. 42,502,635,227 bilioni huku katika mkoa wa Ruvuma wakulima 11,463 wamelipwa Sh. 10,557,222,943 bilioni.
Aidha, Waziri huyo amesema Sh. 101,091,960 milioni imelipwa kwa wakulima 81 katika mkoa wa Pwani na kusisitiza kuwa, vyama vilivyohakikiwa ni 461 na vilivyolipwa ni 451, ambapo jumla ya kilo 40,381,798 zimepatikana.