Home KILIMOKILIMO BIASHARA Maonesho ya kwanza ya kilimo kufanyika mazingira ya jangwa

Maonesho ya kwanza ya kilimo kufanyika mazingira ya jangwa

0 comment 168 views

Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka sekta ya kilimo wanaalikwa kushiriki katika maonesho ya kimataifa ya mazao ya kilimo yatakayofanyika Doha- Qatar.

Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) imesema inaratibu ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo yajulikanayo kama Horticulture Expo Doha 2023.

“Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka sekta ya kilimo wanaalikwa kushiriki ili kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao katika soko la kimataifa.

Pia kukutanishwa na wafanyabiashara na wakulima wa bidhaa za matunda, viungo, na mbogamboga duniani kote kwa lengo la kuwapa fursa wakulima na wazalishaji kubadilishana uzoefu,” inasema taarifa ya TanTrade.

Taarifa hiyo inasema maonesho hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika katika nchi yenye mazingira ya jangwa yanatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 2, 2023 hadi Machi 28, 2024.

“Maonesho hayo pia yatazikutanisha nchi washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kilimo kwenye mazingira ya jangwa,” inaeleza taarifa hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter