Kampuni ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi, Songas imechangia milioni 47 kwenye shule ya msingi Ubungo Kisiwani. Songas imetoa kiasi hicho cha fedha kama mchango wake katika maendeleo ya jamii kwa nia ya kuboresha elimu katika shule hiyo .
Sherehe za ugawaji fedha hizo zilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker pamoja na Mwenyekiti wa mtaa wa kibangu, Desidery Ishengoma na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ubungo Kisiwani.

Mkurugenzi mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya milioni 47 Mwenyekiti wa mtaa wa Kibangu, Bw Desidery Ishengoma katika shule ya msingi Ubungo Kisiwani mapema leo, Kampuni hiyo ya uzalishaji wa gesi nchini Tanzania imetoa msada huo kama mchango wao katika kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Mkurugenzi mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya TZS milioni 47 kwa wanafunzi wa Ubungo Kisiwani mapema leo, Kampuni hiyo ya uzalishaji wa gesi nchini Tanzania imetoa msada huo kama mchango wao katika kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu nchini.