Home VIWANDAMIUNDOMBINU Wananchi 94% wanapata mawasiliano

Wananchi 94% wanapata mawasiliano

0 comment 105 views

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema hadi sasa, serikali imefikisha huduma ya mawasiliano kwa takribani asilimia 94 ya wananchi na kujenga minara 530 maeneo mbalimbali kote nchini. Waziri huyo amesema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano na kuongeza kuwa, sekta hiyo imepelekea taasisi za serikali kutumia mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji mapato na utoaji huduma serikalini na kwa wananchi wa kawaida.

Mhandisi Kamwele ameeleza kuwa ili kuhakikisha sekta ya mawasiliano inaimarika, serikali imekuwa ikishirikiana na sekta binafsi, taasisi mbalimbali na wadau wa shughuli za mawasiliano kwa lengo la kuendeleza matumizi ya huduma za mawasiliano.

“Hadi sasa tuna laini za simu za mkononi zaidi ya milioni 45 na watumiaji wa intaneti wapatao milioni 23, aidha serikali kupitia sekta ya mawasiliano imeendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano katika kudhibiti uhalifu mtandaoni”. Amesema Waziri huyo.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, kwa mwaka wa fedha 2016/2017, sekta ya mawasiliano ilichangia kwa asilimia 13.1 kwenye pato la taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter