Home VIWANDAMIUNDOMBINU Serikali imejipanga ujenzi maghala: Rais Dkt. Mwinyi

Serikali imejipanga ujenzi maghala: Rais Dkt. Mwinyi

0 comment 24 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula ili kuwa na uhakika wa chakula hivyo kujitokeza kwa Sekta binafsi kuanza kujenga ghala ni jambo linalopaswa kuungwa mkono.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo wakati akifungua ghala la Kuhifadhia chakula Gando , Wilaya ya Wete ,Mkoa wa Kaskazini Pemba linalomilikiwa na Kampuni ya Yasser Provision .

Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali inalenga kuwapunguzia mzigo wa gharama wafanyabiashara wanaoleta chakula nchini ili kuwepo kwa unafuu wa bei kwa wananchi.

Rais Dk. Mwinyi ameielezea njia nyengine ni kuwa na ushuru maalum kwa bidhaa zinazopelekwa Pemba .

Rais Dk. Mwinyi amebainisha kuwa mpango wa kuifungua Pemba kiuchumi una dhamira thabiti ya kuhakikisha bei za bidhaa muhimu zinashuka na kutoa unafuu wa maisha kwa wananchi.

Ameeleza kuwa ujenzi wa Bandari za Mkoani, Shumba Mjini na Wete ambao utaanza karibuni ni miongoni mwa hatua muhimu ya kuwawezesha wafanyabishara kuleta mizigo yao moja kwa moja Pemba kutoka nchi wanazoagiza ili kupunguza gharama za mzunguko wa usafirishaji.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali inajipanga kutafuta njia bora za kupunguza gharama za chakula kwa wananchi wa Pemba .

Ufunguzi wa ghala hilo ni miongoni mwa shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter