Home VIWANDA Viwanda visivyoendelezwa kurudi serikalini

Viwanda visivyoendelezwa kurudi serikalini

0 comment 130 views

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema serikali haitasita kuwanyang’anya viwanda wawekezaji ambao wameshindwa kuviendeleza viwanda hivyo na badala yake kuvigeuza kuwa magofu, jambo ambalo amedai linarudisha nyuma harakati za uchumi wa viwanda. Naibu Waziri Manyanya amesema hayo wakati akifungua maonyesho ya wajasiriamali kanda ya kaskazini yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

Mhandisi Manyanya amefafanua kuwa sio sawa wawekezaji hao kupewa viwanda halafu wanashindwa kuviendeleza, huku wakiacha mzigo wa madeni unaolipwa na serikali pekee kwani viwanda vingine vimejengwa mikopo. Naibu huyo ameeleza kuwa lengo la serikali ni kutoa fursa ya ajira na kulipa madeni lakini hali imekuwa tofauti kwa sababu baadhi ya wawekezaji wameshindwa kuviendeleza viwanda hivyo.

“Safari hii hatutakuwa na majadiliano. tunawapokonya viwanda hivyo kwa aibu kama umeshindwa kuendeleza ni heri uvirudishe serikalini kimya kimya lakini ukisubiri tutakichukua kwa aibu. Ukiona ulichukuwa kiwanda kwa hila halafu huna mtaji wa kukiendeleza rejesha ili serikali iweze kuona namna bora ya kuendesha kiwanda hicho na kusaidia watanzania kupata ajira”. Amesema Manyanya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa SIDO, Joyce Meru, amesema katika kutekeleza sera ya viwanda, hado sasa wametengeneza mashine takribani 1,808 zinazosaidia kuongeza thamani bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali. Pamoja na hayo, wametoa mikopo thamani ya Sh. 1.7 bilioni kwa wajasiriamali zaidi ya 2,071 katika kipindi cha mwaka 2017/2018.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter