Home VIWANDA Wamiliki wa viwanda walia na tozo ya sukari

Wamiliki wa viwanda walia na tozo ya sukari

0 comment 95 views

Baadhi ya watumiaji wa sukari kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa za viwandani wametoa malalamiko yao kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutorejesha fedha za tozo ya asilimia 15 wanayotozwa kama dhamana ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kwa wakati unaotakiwa. Malalamiko hayo yametolewa na wamiliki wa viwanda vya kutengeneza vinywaji wakati Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu akitembelea moja ya viwanda jijini Mbeya.

Ofisa Uhusuano wa kiwanda cha SBC Tanzania Limited ambacho kinazalisha vinywaji jamiii ya Pepsi Fort Nyireda amedai kitendo cha mamlaka hiyo ya mapato kuchukua muda mrefu kurejesha fedha hizo viwandani kinapelekea wao kushindwa kujiendeleza na kupanua viwanda vyao. Nyireda ameeleza kuwa hadi sasa, SBC inadai takribani Sh.12 bilioni ambazo anaema endapo zingerejeshwa zingetumika kuendeleza kiwanda hicho katika mikoa mingine.

Akijibu malalamiko hayo, Mama Samia amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa viwanda kupunguza tatizo la ajira hapa nchini kwani watu wengi wanapata ajira kupitia viwanda hivyo. Samia amesema atachukua malalamiko yanayohusu masuala ya kifedha na kuyafikisha kwa wataalamu kabla ya serikali kufanya maamuzi yoyote.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter