Home VIWANDAMIUNDOMBINU Ajali ya moto: Fanya, epuka haya

Ajali ya moto: Fanya, epuka haya

0 comment 123 views

Mara nyingi moto unaotokea katika magari huwa unaweza kuzuiwa ikiwa dereva anaendesha gari kwa usalama na kufanya matengenezo ya gari ya mara kwa mara ili kufanya marekebisho yanayohitajika. Mbali na kufanya hivyo, ni muhimu kujua nini cha kufanya na kutofanya ikiwa moto unawaka katika gari yako au gari uliyopanda ili kuzuia majeraha makubwa na kuokoa maisha.

Mambo ya kufanya

  • Jambo la kwanza na la muhimu kabisa kufanya ikiwa moto unawaka katika gari ni kuwa mtulivu, na onyesha ishara kwa magari yaliyopo nyuma yako kuwa unataka kutoka barabarani.
  • Hata kama huoni moto wala moshi, kama unasikia harufu ya kitu kinaungua ni muhimu kusimamisha na kuzima gari kisha kutoka nje ya gari haraka iwezekanavyo.
  • Kama uko katikati ya barabara kwa mfano kwenye foleni na haiwezekani kupaki gari pembeni, basi simama, washa ishara ya hatari (Hazard), zima gari, toka nje ya kwa uangalifu. Kuhusu magari mengine ni dhahiri kuwa baada ya kuona gari yako inatoa moshi au kuwaka moto wataondoka eneo la tukio na kwenda sehemu yenye usalama zaidi, ikiwa kuna watu karibu basi watahadharishe kuondoka eneo la tukio mara moja kwa ajili ya usalama wao.
  • Unachotakiwa kujali zaidi ni usalama wa maisha yako na si vitu vya thamani kwa sababu wakati unazingatia kutoa vitu hivyo gari linaweza kulipuka. Hivyo acha vitu katika gari na nenda sehemu salama.
  • Baada ya kuhakikisha uko mbali na gari linalowaka moto, piga simu Zimamoto kwa msaada zaidi. Kwa Tanzania namba ya simu ni 114.

Mambo ya kuepuka

  • Jambo la kwanza unalotakiwa kuepuka ni uoga. Hivyo usiogope, kwa sababu kwa kufanya hivyo unaweza kufikia maamuzi yasiyo sahihi ambayo yatapelekea kuhatarisha maisha yako.
  • Mali zipo na zinatafutwa, hivyo epuka kuzingatia zaidi kuokoa mali zilizopo katika gari. Jambo la muhimu kwa wakati huo ni maisha yako.
  • Usijipe moyo kuwa moto umeisha ikiwa ghafla hakuna moshi wala moto unaoonekana. Pia ikiwa moshi unatoka katika boneti ya gari, epuka kufungua boneti hiyo kwa sababu hewa yoyote itakayopita baada ya kufungua boneti na kufikia injini inaweza kusababisha gari kulipuka papo hapo.
  • Epuka kutumia maji kuzima moto kwani maji huchochea moto kutokana na uwepo wa oxygen.
  • Usikae karibu na gari baada ya kutoka nje, kwani gari linaweza kulipuka.
  • Usiendeshe gari kwa kasi ukifikiri kuwa upepo utazima moto mdogo. Kadri upepo unavyoongezeka ndivyo moto nao unavyoongezeka.

Mwisho wa siku ni muhimu kuwa na kifaa cha kuzimia moto kila mahali ikiwa ni pamoja na kwenye gari, ofisini, nyumbani, sehemu za biashara nk ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na ukosefu wa vifaa sahihi vya kuziia moto. Aidha kama una kifaa cha kuzimia moto ni vyema kukifanyia huduma kila inapohitajika ili kuhakikisha kipo tayari pale moto unapotokea. Pia si vibaya kuwatafuta wataalamu ili kupata elimu na kujifunza udhibiti wa moto wa aina mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter