Home VIWANDANISHATI Kamati ya Bunge yatembelea miradi ya umeme kinyerezi

Kamati ya Bunge yatembelea miradi ya umeme kinyerezi

0 comment 103 views
Na Mwandishi wetu

Kamati ya Bunge la Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Hawa Ghasia, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi ambayo inaendeshwa na serikali ili kujiridhisha na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Kamati hiyo ilipokelewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ambaye amewahakikishia kuwa miradi hiyo inaendelea kama serikali ilivyopanga. Vilevile Dk. Kalemani amewataka watanzania kutegemea ongezeko la umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika.

Naibu Waziri pia amesema baada ya mradi wa Kinyerezi I kupanuliwa, kutakuwa na ongezeko la umeme kwa megawati 35, huku mradi wa Kinyerezi II ukitoa megawati 240. Baada ya miradi yote hii kumalizika na kujumlishwa na Kinyerezi III na IV itakayofuata siku za mbele, kutakuwa na jumla ya megawati 1175.

Baada ya kumaliza ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Bajeti alipongeza kazi nzuri inayofanyika na amesema wabunge wanatarajia kuona miradi hii ambayo inagharimu fedha nyingi za walipa kodi ikikamilika ili serikali itekeleze mipango yake ya ujenzi wa viwanda kama ilivyoahidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter