Mfanyabiashara ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MeTL Group, Mohammed Dewji (Mo Dewji) ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 18 wa Afrika kwa ripoti ya mwaka 2022.
Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.5 sawa na Sh3.4 trilioni utajili ambao ni sawa na mwaka jana hivyo hajaongeza wala kupunguza.
Katika orodha ya jarida la Forbes kwa mwaka huu limemtaja MO kuwa bilionea namba 15 akifungana na matajiri wengine wawili Othman Benjelloun na Youssef Mansour wote wakiwa na utajili sawa.
Katika orodha ya jarida hilo mwaka jana Mo ambaye ni raia wa Tanzania anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 15 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.5 (3.4 trilioni).
Kwa kuingia katika orodha hiyo, Dewji anafuata nyayo za mmiliki wa Mamelodi Sundowns, Patrice Motsepe ambae yeye ana utajiri unakadiriwa kufikia Dola 3 bilioni, zaidi ya Sh 9 trilioni.
Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Aliko Dangote mwenye utajiri wa Dola 13.9 bilioni.
Dangote amewekeza katika biashara za sukari na simenti.
Dangote anafuatiwa na Johann Rupert & family mwenye utajiri wa Dola 11 bilioni huku nafasi ya tatu ikishikilia na Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 8.7 bilioni.
Kwa mujibu wa Forbes, Mo ni Mtanzania na mtu pekee kutoka Afrika Mashariki alieingia katika orodha hiyo.
Nchi za Afrika Kusini, Nigeria na Misri zimetajwa kutawala katika orodha hiyo.
Mo Dewji amewekeza katika viwanda vya nguo, unga wa ngano na sembe, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari na vinywaji.
Soma: Mo Dewji: Bilionea kijana zaidi Afrika