Home BIASHARAUWEKEZAJI Dubai Expo kuzalisha ajira 200,000

Dubai Expo kuzalisha ajira 200,000

0 comment 102 views

Tanzania imetia saini hati za makubaliano (MoU) 36 katika mkutano wa biashara na uwekezaji uliofanyika Dubai, Februari 26, 2022.

Hati hizo zinahusisha wizara mbalimbali, taasisi za umma, wawekezaji, sekta binafsi na makampuni mengine.

Kati ya hati hizo 36, hati 12 ni baina ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara na taasisi za umma na wawekezaji mbalimbali.

Hati 23 zimetiwa saini baina ya makampuni binafsi kutoka Tanzania na makampuni mengine yenye nia ya kushirikiana katika sekta mbalimbali za kiuchumi huku hati moja itahusisha Wizara ya Viwanda ya Zanzibar na wawekezaji wanaonuia kushirikiana kwenye sekta ya utalii.

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema kuwa makubaliano hayo pia yatatengeneza takribani ajira 200,000.

“Idadi ya ajira zinazotarajiwa kupatikana kwa ujumla kutokana na makubaliano hayo ni zaidi ya 200,000 katika kipindi cha miaka minne, huku uwekezaji huo ukigharimu zaidi ya dola bilioni 7.49 ambayo ni sawa na shilingi trilioni 17.35 za Kitanzania,” imeandika taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugunzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus.

Taarifa hiyo imezitaja sekta zinazotarajiwa kunufaika na makubaliano hayo kuwa ni nishati, kilimo, utalii, miuondombinu, usafiri, teknolojia na nyinginezo.

Akiongea katika mkutano huo wa Biashara na Uwekezaji, Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili kushawishi uwekezaji na kutengeneza bidhaa madhubuti na za kisasa nchi inahitaji elimu bora.

“Leo naisihi hasa serikali ya UAE nan chi nyingine zinazoshiriki kwenye Expo 2020 Dubai kutoa fursa kwa wanafunzi wa Tanzania kusoma kupitia ufadhili na mpango wa ubadilishanaji wa wanafunzi,” amesema Rais Samia.

Rais amesema “tuna faraja leo tumesaini mikataba ya makubaliano 36, kati ya wafanyabiashara, serikali na wadua wengine. Tunatumaini kwamba kusainiwa kwa mikataba hii hakutaishia tuu kwenye hafla ya kusaini bali itaenda kutekelezwa kwa vitendo.”

Ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania imeweka banda lake katika maonesho ya Dubai Expo hali iliyosaidia kuwepo kwa mikutano mingi iliyokuanisha afanyabiashara wenye lengo la kuwekeza nchini.

 

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter