Home KILIMO Tutawaunganisha wakulima na soko: Rais Samia

Tutawaunganisha wakulima na soko: Rais Samia

0 comment 212 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kujua mahitaji ya bidhaa gani inatakiwa wapi ndani na nje ya nchi.

“Kuna mambo mawili ambayo yana utata na tunayafanyia kazi, kujua biadhaa gani inatakiwa na la pili ni kuunganisha mkulima na soko,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameyasema hayo katika Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika (AGRF) linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Amebainisha kuwa kuunganisha mkulima na soko haijafanywa vizuri bado.

“Tumeanza kufanya kwenye baadhi ya mazao kwa mafano korosho, na tumeshuhudia mara kadhaa bei ya korosho ikipanda kwa sababu tunamkutanisha ushirika wa mkulima pamoja na mnunuaji na kumwondoa mtu wa katikati,” ameeleza Rais Samia.

Amebainisha kuwa hiyo imesaidia kuondoa mtu wa katikati ambae hununua baidhaa kwa mkulima zikiwa shambani kwa bei ndogo.

“Tumeshuhudia hivi karibuni ufuta, tumeuingiza kwa ushirika na kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani, wakulima wanapeleka mazao yao kwenye ushirika, wanunuaji wanashindanishwa na bei inapanda na bidhaa yote inakwenda kwa bei nzuri,” amesema Rais Samia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter