Home KILIMOKILIMO BIASHARA Rais Benki ya Dunia atembelea wakulima wa mwani Zanzibar

Rais Benki ya Dunia atembelea wakulima wa mwani Zanzibar

0 comment 185 views

Rais wa Benki ya Dunia (WB) Ajay Banga Banga, amezungumza na baadhi ya wanufaika wa Mradi wa kilimo cha mwani unaowanufaisha zaidi ya watu 15,000, ambapo asilimia 74 ni wanawake.

Akiwa na waziri wa Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba, wametembelea mradi huo katika kijiji cha Muungoni, Mkoa wa Kusini, Wilaya ya Kusini, Zanzibar, ambao umewezeshwa na Benki ya Dunia kupitia mfuko wa IDA, kwa ajili ya kukuza uzalishaji wa mwani pamoja na kupanua wigo wa upatikanaji wa soko.

Kiongozi huyo wa WB amewahakikishia wakulima hao utayari wa Benki hiyo kusaidia juhudi za Serikali za kuboresha maisha ya wakazi wa Zanzibar kupitia program mbalimbali wanazofadhili.

Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameeleza kuwa programu hiyo imesaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza uzalishaji wa mwani, pamoja na kupunguza gharama na kuboresha maisha yao.

Ziara katika mradi huo ni mwendelezo wa matukio kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid-Term Review) unaohusisha wakopaji, nchi Wahisani na Menejimenti ya Benki ya Dunia, ambao unafanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar unaotarajiwa kuhitimishwa kesho Desemba 8, 2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter