Shirika la ndege la Precision Air linalofanya safari katika mikoa mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi limetangaza ofa mpya kwa wateja waobaada ya kuingia makubaliano na hoteli ya Southern Sun na mgahawa wa Akemi kuwazawadia punguzo la asilimia 20 wasafiri wa mara kwa mara.
Akizungumzia ushirikiano huo. Meneja masoko na mawasiliano wa Precision Air, Hillary Mremi amesema makubaliano hayo yanatekelezwa chini ya programu iitwayo “Paa Royal” ambayo itaweza kuwanufaisha wateja hao kwa kuwapatia kadi maalumu wateja wake
Soma Pia Precision Air yazindua safari za Kahama leo
Likiwa ni shirika la kitanzania lenye wanachama wapatao 20,000 Precision Air imekuwa ikitoa huduma za usafiri wa anga kwa zaidi ya miaka 20 katika sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi hivyo kusaidia katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini.
Akielezea malengo ya kuanzisha mpango huo , Mremi amesema kuwa mpango wa Paa Royal ni kuwafanya wanachama wao kufaidika kupitia pointi wanazopata kwa kusafiri na shirika hilo kama moja ya njia ya kutambua mchango mkubwa wa wanachama na wateja wa shirika hilo.
“Precision Air tunatoa kipaumbele kwa wanachama na wateja wetu kuliko kitu kingine chochote ndio maana mara zote tunahakikisha wanafurahia safari zao wanaposafiri nasi. Ushirikiano wetu na hoteli ya Southern Sun na mgahawa wa Akemi ni mwanzo tu, tutaendelea kuongeza faida nyingi zaidi na zenye tija kwa wateja wetu”. Ameeleza Mremi.
Soma Pia ATCL kuruka nje
Naye Mkurugenzi wa hoteli ya Southern Sun, Michael Phillipson amesema kuwa anafurahi kwa kampuni ya Precision Air kuzikubali kazi zao na kuamua kushirikiana nao kwa kutoa asilimia punguzo la asilimia 20 kwenye vinywaji na chakula pamoja na punguzo la asilimia 10 kwa huduma za malazi hotelini hapo.
“Kwa zaidi ya miaka 17 tumekuwa tujkitoa huduma bora za malazi na chakula nchini. Tukiwa ni moja ya hoteli bora na za kisasa jijini Dar es salaam iliyopo katikati ya jiji”. Amesema Mkurugenzi huyo