Home FEDHAMIKOPO Milioni 600 kuwanufaisha wajasiriamali Njombe

Milioni 600 kuwanufaisha wajasiriamali Njombe

0 comment 93 views

Meneja wa Benki ya NMB  mkoani Njombe, Daniel Zake amesema zaidi ya Sh. 600 milioni zimekopeshwa kwa wajasiriamali mkoani humo baada ya kurasimisha ardhi, hali iliyopelekea kupata mikopo hiyo yenye dhumuni la kuwawezesha wajasiriamali hao kupata mitaji na kuanzisha biashara ili kukuza uchumi. Zake ameeleza kuwa, kazi inayofanywa kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) inalenga kuwainua wajasiriamali wadogo.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum kwenye mafunzo kwa wajasiriamali hao. Meneja huyo ameeleza kuwa, lengo ni kuwajengea uwezo zaidi wajasiriamali ili kuongeza tija katika shughuli wanazofanya na kupanua wigo wa uzalishaji.

“Tunatoa mikopo kwa kutumia leseni za makazi na hati za kimila ambazo wananchi wanapata baada ya kurasimisha maeneo yao na kupimwa na hatimaye kupata hati na katika swala hili, tunapongeza Mpango wa Taifa wa  Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)”. Amesema Zake.

Pamoja na hayo, Meneja huyo amesema wajasiriamali wanaporasimisha biashara zao, mbali na kupanua wigo wa biashara hizo pia wanaongeza masoko, ajira na kuiwezesha serikali kuongeza ukusanyaji wa kodi na mapato kutokana na kukua kwa uzalishaji na shughuli za ujasiriamali kwa ujumla.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter