Home VIWANDA Sido yakabidhiwa majengo viwanda Babati

Sido yakabidhiwa majengo viwanda Babati

0 comment 108 views

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Nchini (Sido) limeanza mchakato wa ujenzi wa majengo maalum kwa ajili ya viwanda vipya mikoa mbalimbali nchini. Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya takribani Sh. 5 bilioni zilizotolewa na Rais Magufuli mwaka jana unalenga kuwawezesha wajasiriamali wadogo wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya viwanda, ambapo mkoa wa Manyara umetumia Sh. 777 milioni kukamilisha ujenzi wa majengo matatu mjini Babati.

Akizungumza wakati wa kukabidhi majengo hayo kwa Prof. Sylvester Mpanduji, Mkurugenzi Mkuu wa Sido, Meneja wa Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), ukanda wa kaskazini, Meja Daudi Zengo amesema mradi huo umekamilika kwa wakati na ni wa aina yake hapa nchini.

Kwa upande wake, Prof. Mpanduji amesema tayari baadhi ya wajasiriamali wawekezaji wameanza kujitokeza na kusisitiza kuwa fursa kama hizo ndio zitakazofanikisha kufikia uchumi wa kati. Naye Meneja wa Sido mkoani Manyara, Abel Mapunda ametoa wito kwa wajasiriamali mkoani humo kuchangamkia fursa ya uwekezaji ili kuongeza tija.

Mbali na mkoa wa Manyara, mikoa mingine ambayo mradi huu unatekelezwa ni Geita, Kagera na Dodoma.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter