Home BENKI BoT kuanza kutumia mfumo wa riba utekelezaji sera ya fedha

BoT kuanza kutumia mfumo wa riba utekelezaji sera ya fedha

0 comment 246 views

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajiwa kuanza kutumia mfumo wa riba katika utekelezaji wa sera ya fedha kuanzia Januari 2024.

Hatua hii inalenga kudhibiti mfumuko wa bei na kuwezesha ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia mazingira ya kiuchumi ya ndani na nje.

Akizungumza katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa BoT jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Missango, amesema kuwa riba hiyo itajulikana kama Riba ya Benki Kuu na itakuwa inatokana na lengo la mfumuko wa bei na makadirio ya ukuaji wa uchumi.

“Riba ya Benki Kuu itatumika kama kigezo cha kuweka viwango vya riba kwa wateja wa benki na taasisi nyingine za fedha nchini,” amesema.

Dkt. Misssango alisema kuwa mabadiliko katika Riba ya Benki Kuu yataonyesha mwelekeo wa sera ya fedha ambapo ongezeko lake litamaanisha kupunguza ujazi wa fedha, wakati kupungua kwa riba hiyo kutamaanisha kuongeza ujazi wa fedha katika uchumi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter