Home BIASHARA Serikali kuwainua wachimbaji wadogo

Serikali kuwainua wachimbaji wadogo

0 comment 103 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali itahakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo na kuwashauri kujiunga katika vikundi ili serikali iwapatie misaada mbalimbali ikiwemo mikopo itakayowaongezea mitaji. Waziri Mkuu amesema hayo wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe. Majaliwa amewataka wachimbaji hao kutumia vizuri taasisi za kifedha zinazowazunguka na kukopa fedha zitakazowawezesha kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji.

Aidha, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kuwa serikali imejipanga kumaliza changamoto ya maji safi na salama na kuongeza kuwa, serikali imetoa zaidi ya Sh. 1 bilioni kwa ajili ya kuchimba visima virefu 11 na vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

“Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Mbogwe wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao”. Amesema Majaliwa.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema wilaya hiyo inafanya vizuri katika sekta ya madini, ikiwa na viwanda 27 vya kuchenjulia dhahabu. Aidha Biteko ameeleza kuwa, serikali imetenga eneo la hekta 547.64 kwa ajili ya wachimbaji hao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter